Sambamba na kuwadia kwa maadhimisho ya kuzaliwa kwa binti wa Bwana wa Wachamungu, bendera yenye jina la Mtukufu Zaynab (amani iwe juu yake) ilipeperushwa juu ya Iwan ya Najaf, na uwanja na maeneo ya haram tukufu ya Imam Ali yakapambwa kwa mabango ya kuzaliwa kwake.








