Aya hii imeteremshwa kuhusu fadhila za Amir al-Mu’minin (a.s), kwa sababu yeye alijitolea maisha yake na mali yake katika njia ya Uislamu na alikuwa mfano kamili wa mpiganaji katika njia ya Mungu.
Sura An-Nisa, Aya ya 95
« لا يَسْتَوِي الْقاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ وَ الْمُجاهِدُونَ في سَبيلِ اللهِ بِأَمْوالِهِمْ وَ أَنْفُسِهِمْ فَضَّلَ اللهُ الْمُجاهِدينَ بِأَمْوالِهِمْ وَ أَنْفُسِهِمْ عَلَى الْقاعِدينَ دَرَجَةً وَ كُلاًّ وَعَدَ اللهُ الْحُسْنى وَ فَضَّلَ اللهُ الْمُجاهِدينَ عَلَى الْقاعِدينَ أَجْراً عَظيماً »
Imam Hadi (a.s), katika siku ya sikukuu ya Ghadir, alimzuru babu yake mtukufu, Amir al-Mu’minin (a.s), kwa Ziyarat ya Ghadir. Katika sehemu ya Ziyarat ya Ghadir imesemwa: « Wewe ni yule ambaye Qur’ani imeshuhudia ubora wake; Mungu Mkuu na Mtukufu amesema: “Na Mwenyezi Mungu amewafadhilisha wale wanao pigania Dini kwa mali zao na nafsi zao kuliko wale wanao kaa [bila sababu]; [fadhila hiyo ni] daraja kutoka kwake, na msamaha [maalum] na rehema [maalum]; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” (An-Nisa/95). »
Aya ya 95 ya sura ya An-Nisa inazungumzia tofauti ya daraja kati ya wale wanaopigana katika njia ya Mungu na wale wasiopigana, na inafafanua fadhila za wapiganaji. Aya hii ni mojawapo ya “Aya za Alawiyya” ndani ya Qur’ani Tukufu zinazoashiria fadhila za Amir al-Mu’minin (a.s), kwa sababu anatambulika kama mmoja wa wapiganaji mashuhuri katika njia ya Uislamu.
Imam Hassan al-Askari (a.s), akinukuu kutoka kwa baba yake Imam Hadi (a.s), katika riwaya inayorejelea aya hii na jihadi ya Amir al-Mu’minin (a.s), alisema:
« Unapokusudia kumzuru Amir al-Mu’minin (a.s), simama mbele ya lango la kuba tukufu na sema: … Ninashuhudia kwamba wewe kwa hakika ni Amir al-Mu’minin (a.s), ambaye aya za Mungu zimeteremshwa kumhusu. Wewe ni Wali wa Mungu, ndugu yake Mtume wake, na mtetezi wa dini ya Mungu. Wewe ni yule ambaye Qur’ani imeshuhudia ubora wake, na Mungu amesema: “فَضَّلَ اللهُ المُجاهِدِینَ عَلَی الْقاعِِدِینَ أَجْراً عَظِیماً دَرَجاتٍ مِنْهُ وَ مَغْفِرَةً وَ رَحْمَةً وَ کانَ اللهُ غَفُوراً رَحِیما.” »
Chanzo
Tafsir Ahl al-Bayt (a.s), Juzuu ya 3, uk. 386, Bihar al-Anwar, Juzuu ya 97, uk. 363