Most searched:

Uongofu wa Kiungu katika Wilayah

Uongofu wa Kiungu Unategemea Wilayah ya Amirul Muuminina (a.s)

Dhana ya “uongofu” katika aya ya 8 ya Surah Al Imran kwa Ahlul-Bayt, inahusiana na Wilayah ya Amirul Muuminina (a.s). Kulingana na baadhi ya riwaya, mwongozo na uongofu wa kweli baada ya Hitimisho la Manabii, unawezekana tu kwa kushikamana na Wilayah ya Amirul Muuminina (a.s) na Maimamu maasumu.

Aya ya 8 ya Surah Al Imran
 «رَبَّنا لاتُزِغْ قُلُوبَنا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنا وَ هَبْ لَنا مِنْ لَدُنْكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنْتَ الْوَهّابُ»

Kwa mujibu wa riwaya ya Imamu Hadi (a.s) katika Ziyara ya Ghadiriyyah, aya hizi ni ukumbusho wa nafasi ya juu ya Amirul Muuminina (a.s).

Katika sehemu ya Ziyara ya Ghadiriyyah inasema:
«Basi hawakuamini yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kumhusu wewe kwa nabii Wake isipokuwa watu wachache tu, na kwa walio wengi haikuwazidishia chochote isipokuwa hasara. Kabla ya hapo pia Mwenyezi Mungu alikuwa ameteremsha aya hii kuhusu haki yako, ingawa wao hawakupenda hilo: “(Hawa husema) Mola wetu Mlezi! Usizipotoshe nyoyo zetu baada ya kutuongoza! Na utupe rehema kutoka Kwako; hakika Wewe ndiye Mpaji Mkuu.”»

Yaliyomo zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *