Leo katika sehemu ya “Aya za Alawiyya” na katika video mnayoitazama, imezinduliwa moja ya athari za ki qurani za “Maonyesho ya Picha ya Uandishi wa Aya za Alawiyya” ambayo imeandikwa na mmoja wa maprofesa wa sanaa asili ya kaligrafia (hati nuri) katika kuelezea daraja ya juu ya Amirul Mu’minin Ali (A.S).
Aya inayozungumziwa leo ni aya ya 274 ya Surah Al-Baqarah:
Mwenyezi Mungu katika aya ya 274 ya Surah Al-Baqarah anasema:
«الَّذينَ يُنْفِقُونَ أَمْوالَهُمْ بِاللَّيْلِ وَ النَّهارِ سِرًّا وَ عَلانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَ لا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَ لا هُمْ يَحْزَنُونَ؛ Wale ambao hutoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri, basi wana ujira wao kwa Mola wao, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.»
Aya hii ambayo inajulikana kama Aya ya Infaq (Aya ya Kutoa), inahusu wale wanaotoa mali zao usiku au mchana, kwa siri au dhahiri, na ni miongoni mwa aya zilizoshuka kuhusu ukubwa wa Hazrat Amirul Mu’minin Ali (A.S).
Mtume wa Mwisho (S.A.W.W)
Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.W) alisema: “Ewe Ali! Ulifanya nini usiku wa jana?”
Hazrat Amirul Mu’minin (A.S) akasema: “Ewe Mtume wa Mungu (S.A.W.W) kwa nini unauliza?” Yeye akajibu: “[Kwa sababu] nafasi nne tukufu zilishuka kuhusu wewe.”
Hazrat akasema: “Baba na mama yangu wafe kwa ajili yako! Nilikuwa na dirham nne, nikatoa moja usiku, moja mchana, moja kwa siri na nyingine kwa dhahiri.”
Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.W) akasema: “Mwenyezi Mungu ameshusha kuhusu wewe: الَّذِینَ ینفِقُونَ أَمْوَالَهم بِاللَّیلِ وَالنَّهارِ سِرًّا وَعَلاَنِیةً فَلَهمْ أَجْرُهمْ عِندَ رَبِّهمْ وَلاَ خَوْفٌ عَلَیهمْ وَلاَ همْ یحْزَنُونَ.”[1]
Mtume Mtukufu (S.A.W.W) akasema: “Aya ya: الَّذِینَ یُنْفِقُونَ أَمْوالَهُمْ بِاللَّیْلِ وَ النَّهارِ سِرًّا وَ عَلانِيَةً; ilishuka kuhusu ukubwa wa Amirul Mu’minin Ali (A.S).”[2]
Imamu Muhammad al-Baqir (A.S)
Imamu al-Baqir (A.S) amesema: “Aya hii ilishuka kuhusu Ali bin Abi Talib (A.S). Alikuwa na dirham nne, akatoa sadaka dirham moja usiku, dirham moja mchana, dirham moja kwa siri na dirham nyingine kwa dhahiri.”[3]
Ibn Abbas (R.A)
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Abbas: “Aya ilishuka kuhusu Ali bin Abi Talib (A.S). Kwani yeye alitoa dirham nne; katika giza la usiku dirham moja, katika mwanga wa mchana dirham moja, dirham moja kwa siri na dirham nyingine kwa dhahiri.
[Na kwa ajili hiyo] aya hii ilishuka, Mtume (S.A.W.W) akasema: Ni nani miongoni mwenu aliyetoa namna hii? Watu walinyamaza [wasijibu].
Kisha Hazrat akarudia swali na safari hii Ali bin Abi Talib (A.S) akasimama na kusema: Ni mimi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.W), kisha Mtume wa Mwisho akasoma aya ‘فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ’.”[4]
Ibn Abbas akasema: “«وَ لا خَوْفٌ عَلَیْهِمْ وَ لا هُمْ یَحْزَنُونَ» yaani hawaogopi adhabu na kifo wala hawatahuzunika; yaani watakuwa hivyo huko Akhera.”[5]
Tazama Kumbukumbu ya Aya za Alawiyya
Vyanzo
[1] Tafsir ya Ahlul-Bayt (A.S) Jz 2, uk 382 / Bihar al-Anwar, Jz 40, uk 104
[2] Tafsir ya Ahlul-Bayt (A.S) Jz 2, uk 382 / Bihar al-Anwar, Jz 41, uk 35 / Uyun Akhbar al-Rida Jz 2, uk 62
[3] Tafsir ya Ahlul-Bayt (A.S) Jz 2, uk 382 / Ta’wil al-Ayat al-Zahirah, uk 104 / Shawahid al-Tanzil, Jz 1, uk 147 / Furat al-Kufi, uk 71 / Shawahid al-Tanzil, Jz 1, uk 149
[4] Tafsir ya Ahlul-Bayt (A.S) Jz 2, uk 382 / Bihar al-Anwar, Jz 41, uk 33
[5] Tafsir ya Ahlul-Bayt (A.S) Jz 2, uk 384 / Bihar al-Anwar, Jz 41, uk 33