Ujumbe wa Atabatu Tukufu Alawiyya nchini Pakistan uliwapongeza na kuwashukuru baadhi ya shakhsia za kidini, rasmi na kijamii kutoka madhehebu mbalimbali ambao walichangia kufanikisha mipango ya “Wiki ya Kimataifa ya Swaadiqain”.
Mpango huu ulifanyika katika mji wa Lahore, makao makuu ya jimbo la Punjab, kwa lengo la kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu wa Uislamu (rehema na amani za Allah ziwe juu yake na Aali zake) na mjukuu wake, Imam Ja’far al-Swaadiq (amani iwe juu yake).













