Katika mfumo wa mipango ya toleo la tano la “Wiki ya Kimataifa ya Swaadiqain”, mji wa Lahore, ambao ni makao makuu ya jimbo la Punjab na mji wa pili kwa ukubwa nchini Pakistan, ulishuhudia hafla ya kuinua bendera ya Mtume Mtukufu (rehema na amani za Allah ziwe juu yake na Aali zake). Hafla hiyo ilifanyika kwa kuhudhuriwa na ujumbe uliotumwa na Atabatu Tukufu ya Alawiyya na kwa uratibu wa Taasisi ya Minhaj al-Hussein (amani iwe juu yake).
Hafla ya kuinua bendera ilihudhuriwa kwa wingi na viongozi, shakhsia za kidini na makundi mbalimbali ya jamii kutoka madhehebu tofauti. Hafla hiyo iliunda mazingira ya furaha na shangwe yaliyoakisi upendo na utiifu kwa Mtume Mtukufu wa Uislamu (rehema na amani za Allah ziwe juu yake na Aali zake) na Imam Ja’far al-Swaadiq (amani iwe juu yake).
Hafla hiyo ilifanyika katika mfumo wa mpango wa ujumbe wa Atabatu Tukufu Alawiyya, ukiongozwa na Karrar al-Khafaji, Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini, kwa kushirikisha baadhi ya watumishi kutoka Idara za Mahusiano ya Umma, Habari na Masuala ya Kidini za Atabatu.
Ujumbe huo umesafiri kwenda Pakistan kwa lengo la kuadhimisha mipango ya “Wiki ya Swaadiqain” katika miji kadhaa ya nchi hiyo, kupanua mawasiliano na taasisi pamoja na shakhsia za kidini na kijamii, na kuwatambulisha watumishi wa Amirul Muuminiin (amani iwe juu yake) katika minasaba hii.











