Katika mwanzo wa mazungumzo kuhusu “Aya za Alawiyya” zinazotambulisha shakhsia adhimu ya Hazrat Amirul Mu’minin (A.S), na kwa mnasaba wa kumbukumbu ya vita vya Tabuk, tutaashiria aya iliyoshuka kwa Mtume wa Mwisho wa Rehema wakati akirejea kutoka kwenye vita hivi, ambapo alitangaza kuwa dhihirisho lake halisi ni Hazrat Amirul Mu’minin (A.S).
Aya inayozungumziwa leo ni aya ya 41 ya Surah Al-Hijr:
Mwenyezi Mungu amesema: «قَالَ هَذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ»
(Mwenyezi Mungu akasema: “Hii ni njia iliyonyooka ambayo kuilinda ni wajibu wangu, na ni sunna yangu ya daima.”)
Abu Barzah amesema: Tulikuwa tumeketi mbele ya Mtume Mtukufu (S.A.W.W). Yeye aliashiria upande wa Amirul Mu’minin Ali (A.S) na akasoma aya hii:
«وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ» (Al-An’am/153)
(Na kwa hakika hii ndiyo njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni; wala msifuate njia nyingine, zikawatenganisha na njia yake. Haya amewausia ili mpate kuwa wachamungu.)
Mtu mmoja akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.W), kwani makusudio ya aya hii si kwamba Mungu ameikuza njia hii juu ya njia zote [yaani Uislamu]?”
Mtume Mtukufu (S.A.W.W) akasema: “Huu ni dhuluma unaofanya [kuhusu Ali (A.S)]. Ama ulichosema kuwa Mwenyezi Mungu ameupea Uislamu ubora juu ya dini nyingine ni sahihi, lakini aya hii: هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا; ilishuka wakati mimi nikirudi kutoka vita vya kwanza vya Tabuk.”
Nikasema: “Mola wangu, mimi nimemwacha Ali (A.S) miongoni mwa umma wangu kama hiyari ya Haruni (A.S) kwa Musa (A.S); isipokuwa tu hakuna mtume baada yangu. Ewe Mwenyezi Mungu, thibitisha neno langu na utimize ahadi yangu na utaje jina la Ali (A.S) katika Kurani kama ulivyotaja jina la Haruni.”
Kisha Mtume Mtukufu (S.A.W.W) akasoma aya kutoka kwenye Kurani na akasema: “Mwenyezi Mungu amethibitisha neno langu kwa aya hii: قَالَ هَذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ. Yeye ndiye huyu aliyeketi pembeni yangu. Sikizeni ushauri wake na mtiini. Atakae enda kinyume na mimi amemuasi Mungu, na atakae kwenda kinyume na Ali (A.S) ameenda kinyume na mimi.”
Tafsir ya Ahlul-Bayt (A.S) Jz 7, uk 506 / Furat Al-Kufi, uk 137
Vita vya Tabuk na Kutangazwa kwa Imamu wa Amirul Mu’minin (A.S)
Moja ya vita vya Mtume (S.A.W.W) ni vita vya Tabuk vilivyotokea tarehe mosi ya mwezi wa Ramadhani mwaka wa 9 Hijiria. Katika vita hivi, kwa sababu ya kufika kwa habari za harakati za kijeshi za Waroma dhidi ya Waislamu kwa Mtume (S.A.W.W), aliamuru kujiandaa kwa vita. Miongoni mwa matukio muhimu ya vita hivi ni amri ya Mtume (S.A.W.W) kwa Amirul Mu’minin (A.S) kubaki Madina.
Tukio ambalo lilipelekea Mtume (S.A.W.W) kutoa kauli kuhusu Amirul Mu’minin (A.S) ambayo ilikuja kujulikana kama Hadithi ya Manzilat (Hadithi ya Nafasi).
Hadithi ambayo ndani yake nafasi na vyeo vyote vya Haruni (A.S) kwa Musa (A.S) isipokuwa utume, vithibitishwa kwa Amirul Mu’minin (A.S) kwa uwiano na Mtume wa Uislamu (S.A.W.W).
Mtume wa Mwisho (S.A.W.W)
Mtume Mtukufu (S.A.W.W) aliashiria kwa Amirul Mu’minin (A.S) na akasema:
“Na kwa hakika hii ndiyo njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni; na muepuke kufuata njia za kando na potofu zikawatenganisha na njia ya haki. Haya amewausia Mwenyezi Mungu ili mpate kuwa wachamungu.”
Imamu al-Sadiq (A.S)
Hisham bin Hakam amepokea kutoka kwa Imamu al-Sadiq (A.S) kwamba Imamu (A.S) alisoma aya: قَالَ هَذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ, na akasema:
“Alikuwa akimkusudia Ali bin Abi Talib (A.S), yaani hakuna upotovu wowote katika mwenendo wake na dini yake.”
Tafsir ya Ahlul-Bayt (A.S) Jz 7, uk 506 / Ta’wil al-Ayat al-Zahirah, uk 252
Imamu al-Baqir (A.S)
Salam bin Mustanir Al-Ju’fi amesema: Nilienda kwa Imamu al-Baqir (A.S) na nikamuuliza: “Ni nini maana ya aya: قَالَ هَذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ?”
Akasema: “Ni njia ya Ali bin Abi Talib (A.S).”
Tafsir ya Ahlul-Bayt (A.S) Jz 7, uk 506 / Furat Al-Kufi, uk 225 / Basa’ir al-Darajat, uk 512 / Nur al-Thaqalayn / Al-Burhan