Most searched:

Atabatu Tukufu ya Alawi Yaandaa Mipango Maalumu ya Kitamaduni kwa Watoto katika Siku za Kuzaliwa kwa Mtume wa Mwisho

Kituo cha Utamaduni wa Watoto cha “Mohsen” cha Atabatu Tukufu ya Alawi kiliandaa mipango ya kielimu na burudani katika mpango wa “Wiki ya Swaadiqain”.

Katika mpango wa “Wiki ya Swaadiqain”, Kituo cha Utamaduni wa Watoto cha “Mohsen” kinaendelea kuimarisha malezi na fikra za watoto kwa kuandaa mipango na shughuli mbalimbali zenye malengo maalumu. Mipango hiyo ilifanyika katika dandali ya hafla na burudani kwenye Mapumziko ya Ghadir, kwa ushiriki wa zaidi ya watoto 250 wa kike na wa kiume.

Murtadha Abdul-Jawad Kadhim, mkurugenzi mtendaji wa miradi ya kitamaduni ya Kituo cha Mohsen, alisema katika mahojiano na Kituo cha Habari: “Mipango hii, inayoendelea kwa siku tatu, inajumuisha vipindi na shughuli mbalimbali shirikishi, zikiwemo maonyesho ya vikaragosi, ushiriki na maonyesho ya watoto, mashindano ya mtandaoni na kipengele cha hadithi fupi. Pia kuna shughuli mbalimbali za kimwili, kiakili na kifikra ambazo, sambamba na kuleta furaha na burudani, zina vipengele vya kielimu na manufaa.”

Aliongeza: “Mipango hii inalenga kuwafahamisha watoto kuhusu shakhsia ya Mtume Mtukufu Hazrat Muhammad (Rehema na amani za Allah ziwe juu yake na Aali zake) na maadili kama rehema na tabia njema yaliyojitokeza katika sera yake. Pia, mipango hii inatilia mkazo sera ya Imam Jaafar Swaadiq (Amani iwe juu yake), pamoja na mafunzo na maadili ya kimalezi na kifikra yaliyomo ndani yake.”

Shughuli za Kituo cha Utamaduni cha “Mohsen” zimeundwa kwa lengo la kubadilisha maadili na mafundisho yanayotokana na sera hizi mbili zenye nuru kuwa dhana na tabia zinazotekelezeka na vitendo, ili zichangie katika kurekebisha mwenendo wa watoto, kujenga haiba zao na kuimarisha maadili ya Kiislamu na kibinadamu ndani yao. Mipango hii inatekelezwa kwa kutumia mbinu za kisasa za malezi zinazolingana na umri na maslahi ya watoto.

Yaliyomo zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *