Most searched:

Uzinduzi wa Jengo la Kielimu na Atabatu Tukufu Alawiyya

Atabatu Tukufu Alawiyya ilizindua jengo la kielimu sambamba na kufanyika kwa Wiki ya Swaadiqayn.

Msimamizi wa Atabatu Tukufu ya Alawiyya, akiwakilishwa na Bodi ya Elimu ya Alawiyya, alizindua jengo la Shule za Alawiyya sambamba na kufanyika kwa shughuli za Wiki ya Swaadiqayn, zinazoandaliwa kwa munasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu Muhammad (swalla Allahu alayhi wa aalihi) na mjukuu wake mtukufu, Imam Ja’far al-Swaadiq (amani iwe juu yake). Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi na watu mashuhuri wa serikali, sekta ya elimu, vyuo vikuu na jamii.

Hafla ya uzinduzi wa jengo hilo ilihudhuriwa na Yusuf Kanawi, Gavana wa Najaf Ashraf, Hussein al-Isawi, Mwenyekiti wa Baraza la Mkoa, huku ikifanyika kwa udhamini na kuhudhuria kwa Ihsaan Twaa’i, Naibu Msimamizi wa Haram Tukufu ya Alawiyya. Pia walihudhuria wajumbe wa Baraza la Uongozi na wakuu wa idara mbalimbali.

Hafla hiyo ilianza kwa hotuba ya Msimamizi wa Haram Tukufu ya Alawiyya, iliyosomwa na Mustwafaa Munii, mjumbe wa Baraza la Uongozi. Katika hotuba hiyo, alisisitiza umuhimu wa elimu na nafasi yake katika kujenga utu wa mwanadamu, akisema: “Shule ni mazingira ya kupata elimu, uwanja wa malezi na msingi wa kukuza maadili.”

Aliongeza kuwa kuhusishwa kwa shule hizi na Atabatu Tukufu ya Alawiyya kunazidisha wingi wa wajibu wake wa kuimarisha elimu na maadili na kukuza azma kubwa ndani ya wanafunzi.

Katika hafla ya uzinduzi, viongozi kadhaa wa serikali pia walitoa hotuba na kupongeza nafasi ya Atabatu Tukufu ya Alawiyya katika kuunga mkono sekta ya elimu katika Mkoa wa Najaf Ashraf na kuboresha mazingira ya kielimu; hatua inayolenga kulea kizazi chenye elimu na ujuzi na kilichopambwa kwa maadili mema.

Murtadhaa al-Hammaami, msemaji rasmi wa Bodi ya Elimu ya Alawiyya, alisema: “Shughuli za bodi hii hazikomei tu katika kusimamia kundi la shule, bali bodi hii ni mfumo jumuishi wa elimu na malezi unaolenga kujenga utu wa mwanafunzi, kugundua vipaji vyake na kuchangia katika kuunda mustakabali tofauti katika uwanja wa elimu na malezi.”

Yaliyomo zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *