Idara ya nyumba ya wageni ya wafanyaziara ya Atabatu Alawiyya Tukufu, kuanzia tarehe saba ya mwezi wa Swafar katika mwelekeo wa mipango ya mapema kwa ajili ya kutoa huduma kwa wafanyaziara wa Arbaeen, ilianza usambazaji wa chakula kilichobarikiwa miongoni mwa wafanyaziara wa Arbaeen ya Aba Abdillah Al-Hussein (Amani iwe juu yake) ambao wanapata sharafu ya kuzuru Haram tukufu ya kiongozi wa wacha Mungu na kisha kuelekea Karbala tukufu.
Athir Al-Tamimi, mkuu wa idara ya nyumba ya wageni ya wafanyaziara ya Atabatu Alawiyya Tukufu, katika mahojiano na Kituo cha Habari cha Atabatu alisema: “Sambamba na kuwasili mapema kwa mamilioni ya wafanyaziara katika Haram tukufu ya Amirul Muuminiin (Amani iwe juu yake), kuwakarbisha na kuwahudumia kwao kumeanza kupitia kiingilio kikuu cha jengo kuu la nyumba ya wageni ya wafanyaziara, karibu na uwanja wa Sayyida Fatima (Amani iwe juu yake).
Vilevile, sambamba na kumbukumbu ya shahada ya mkarimu wa Ahlul-Bayt, Imam Hassan (Amani iwe juu yake), karamu ya ukarimu wa Alawi imeandaliwa kwa ajili ya wafanyaziara.”
Aliongeza: “Kwa agizo la Uongozi wa Atabatu Alawiyya Tukufu, vituo kadhaa vya utoaji huduma, ukarimu na mapumziko ya wafanyaziara wa Arbaeen vimeanza shughuli zao tangu siku za mwanzo kabisa.
Vituo hivi vinajumuisha vituo vinavyozunguka uwanja mtukufu wa Haidari, maeneo katika njia zinazoelekea kwenye Haram ya Amirul Muuminiin (Amani iwe juu yake) katika sehemu ya kihistoria ya mji wa Najaf al-Ashraf na pia vituo vya huduma katika njia ya matembezi ya Arbaeen; njia ambayo mamilioni ya wafanyaziara katika kuelekea Karbala tukufu wanapita kutoka mji wa Najaf al-Ashraf.”
Inafaa kuashiria kuwa Atabatu Alawiyya Tukufu, kwa kutumia uwezo na idara zake zote, inashiriki katika kutoa huduma kwa wafanyaziara wa Arbaeen ya Aba Abdillah Al-Hussein (Amani iwe juu yake); wafanyaziara ambao wanaichagua Haram tukufu ya Amirul Muuminiin (Amani iwe juu yake) mjini Najaf al-Ashraf kama mojawapo wa vituo vikuu vya njia yao kuelekea Karbala tukufu kwa ajili ya matembezi ya Arbaeen.




