Most searched:

Fadhila za Kusoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu katika Mwezi wa Qur’ani

Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kila siku tunasikiliza kwa makini neno la thamani kutoka kwa Mkuu wa Ufasaha, Amirul Muuminina (a.s) kuhusiana na mwezi huu uliojaa baraka; ili nuru ya maneno yake matukufu iwe mwongozo kwetu katika kufaidika zaidi na baraka za mwezi huu wa utiifu kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa kuanza kwa mwezi wa mapenzi na ibada, mwezi mtukufu wa Ramadhani, hadithi kutoka kwa Amirul Muuminina Ali (a.s) kuhusiana na mwezi huu wa baraka zimekusanywa kwa ajili yenu, wasomaji waheshimiwa, na zitachapishwa kila siku chini ya anwani “Hadithi za Alawi” katika sehemu maalum ya Ramadhani Tukufu.

Hadithi ya siku ya kumi na sita

Amirul Muuminina (a.s) alisema:

“Ewe mfungaji! Jikurubishe kwa Mwenyezi Mungu usiku wako na mchana wako kwa kusoma kitabu Chake, kwani hakika kitabu cha Mwenyezi Mungu ni muombezi ambaye maombezi yake hukubaliwa Siku ya Kiyama kwa wasomaji wake, na kwa kusoma aya zake, wanapanda katika daraja za Pepo.”

أيها الصائم تقرب إلى الله بتلاوة كتابه في ليلك و نهارك فإن كتاب الله شافع مشفع يوم القيامة لأهل تلاوته فيعلون درجات الجنة بقرائة آياته

Chanzo
Fada’il al-Ashhur al-Thalatha, Sheikh Saduq, uk. 108

Imenukuliwa kutoka kwenye khutba ya Amirul Muuminina (a.s) katika siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani