Most searched:

Mwezi wa Ramadhani, Mwezi wa Kujibiwa Dua

Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kila siku tunasikiliza kwa makini neno la thamani kutoka kwa Mkuu wa Ufasaha, Amirul Muuminina (a.s) kuhusiana na mwezi huu uliojaa baraka; ili nuru ya maneno yake matukufu iwe mwongozo kwetu katika kufaidika zaidi na baraka za mwezi huu wa utiifu kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa kuanza kwa mwezi wa mapenzi na ibada, mwezi mtukufu wa Ramadhani, hadithi kutoka kwa Amirul Muuminina Ali (a.s) kuhusiana na mwezi huu wa baraka zimekusanywa kwa ajili yenu, wasomaji waheshimiwa, na zitachapishwa kila siku chini ya anwani “Hadithi za Alawi” katika sehemu maalum ya Ramadhani Tukufu.

Hadithi ya siku ya kumi na tano

Amirul Muuminina (a.s) alisema:

“(Ramadhani) ni mwezi ambao muito husikiwa ndani yake, na dua hujibiwa ndani yake, na kilio huhurumiwa ndani yake.”

هو شهر يسمع فيه النداء و يستجاب فيه الدعاء و يرحم فيه البكاء.

Chanzo
Fada’il al-Ashhur al-Thalatha, Sheikh Saduq, uk. 108

Imenukuliwa kutoka kwenye khutba ya Amirul Muuminina (a.s) katika siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani