Yafuatayo ni kiasi kidogo sana na muhtasari wa kauli za wanachuoni wa Kisunni zilizotajwa kuhusu kuzaliwa kwa Amirul Mu’minin (A.S) ndani ya Kaaba Tukufu, jambo linaloonyesha fadhila zake za kipekee ambazo hazina mfano:
- Al-Fakihi (aliekufa mwaka 275 Hijiria) katika kitabu chake “Akhbar Makkah” anasema: “Mtu wa kwanza kuwa mzaliwa wa Kaaba ni Ali bin Abi Talib (A.S) kutoka Bani Hashim na Wahajiri.”[1]
- Al-Qaffal Al-Shashi Al-Shafi’i (aliekufa mwaka 365 Hijiria) katika kitabu chake “Fadhail Amirul Mu’minin” pia amesema: “Hakuna mtu aliyezaliwa ndani ya Kaaba isipokuwa Ali (A.S).”[2]
- Al-Hakim Al-Nishaburi (aliekufa mwaka 405 Hijiria), mwanachuoni wa Kisunni na mwenye kuaminiwa katika madhehebu ya Sunni, katika kitabu chake maarufu sana “Al-Mustadrak ala Al-Sahihain” anasema: “Riwaya zimekuja kwa sifa ya mutawatir kwamba Fatima bint Asad alimzaa Amirul Mu’minin Ali bin Abi Talib (Karramallahu Wajhahu) ndani ya nyumba ya Kaaba.”[3]
- Al-Allamah Al-Basti Al-Mu’tazili (aliekufa mwaka 420 Hijiria) katika kitabu chake “Al-Maratib” amesema hivi: “Yeye ana sifa ya kipekee msikitini (miongoni mwa waswali wote) ambayo hakuna mtu mwingine anayo, nayo ni kwamba yeye ni mzaliwa wa Kaaba.”[4]
- Ibn Al-Maghazili Al-Maliki (aliekufa mwaka 483 Hijiria) amethibitisha kuzaliwa kwa Amirul Mu’minin (A.S) ndani ya Kaaba na amesimulia kisa cha kuzaliwa huku kwa ukamilifu.[5]
- Ibn Shuja’ Al-Mawsili Al-Shami (aliekufa mwaka 646 Hijiria) katika kitabu chake “Na’imul Muqim” amesema hivi: “Alizaliwa ndani ya Kaaba Tukufu na hakuna mtu yeyote isipokuwa yeye aliyewahi kuzaliwa katika sehemu hii hadi sasa.”[6]
- Sibt Ibnul Jauzi Al-Hanafi (aliekufa mwaka 654 Hijiria) mwanachuoni wa Kisunni, naye katika kitabu cha “Tazkiratul Khawas” ameashiria jambo hili akieleza: “Hazrat huyo alizaliwa ndani ya Kaaba.”[7]
- Al-Allamah Al-Juwayni Al-Shafi’i (aliekufa mwaka 730 Hijiria) katika “Fara’idus Simtain” amesema hivi: “Hakuna mtu isipokuwa Ali (A.S) aliye mzaliwa wa Kaaba.”[8]
- Al-Dhahabi (aliekufa mwaka 848 Hijiria) naye amesisitiza tukio hili, pamoja na kwamba amethibitisha usahihi wake kutoka kwa Al-Hakim Al-Nishaburi na nukuu yake ya mutawatir kuhusu kuzaliwa kwa Amirul Mu’minin (A.S) ndani ya Kaaba.[9]
- Diyar Bakri (aliekufa mwaka 982 Hijiria) katika kitabu chake cha historia kinachojulikana kama “Tarikhul Khamis” ameandika: “Ali bin Abi Talib (A.S) alizaliwa ndani ya Kaaba miaka thelathini baada ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (S.A.W.W).”[10]
- Ali al-Qari Al-Hanafi (aliekufa mwaka 1014 Hijiria) baada ya kuashiria madai ya “Hakim bin Hizam” kuhusu kuzaliwa kwa Amirul Mu’minin (A.S) amesema hivi: “Hakuna mtu yeyote isipokuwa yeye (Amirul Mu’minin (A.S)) anayechukuliwa kuwa mzaliwa wa Kaaba.”[11]
- Burhanuddin Al-Halabi Al-Shafi’i (aliekufa mwaka 1044 Hijiria) katika wasifu wake unaojulikana kama “Al-Sirah Al-Halabiyyah” chini ya mada mbili ameashiria kuzaliwa kwa Amirul Mu’minin (A.S) ndani ya Kaaba.[12]
- Shah Waliyyullah Al-Dahlawi Al-Hanafi (aliekufa mwaka 1176 Hijiria) mwanachuoni wa Kisunni, katika kitabu chake “Izalatul Khafa” amebainisha wazi hivi: “Kulingana na kauli na riwaya za mutawatir, Fatima bint Asad alimzaa Amirul Mu’minin (A.S) ndani ya Kaaba … ambapo kabla na baada ya Hazrat huyo hakuna mtu aliyezaliwa katika sehemu hiyo.”[13]
- Al-Allamah Al-Alusi, mufasiri na mwanafasihi wa madhehebu ya Shafi’i, katika kufafanua ubeti huu wa shairi la mshairi wa Al-Hanafi “Abdulbaqi Al-Amari”, ana kauli isemayo:
- وَأَنْتَ العَلِيُّ الَّذِي فَوْقَ العُلَا رُفِعَا بِبَطْنِ مَكَّةَ عِنْدَ البَيْتِ إِذْ وُضِعَا
- Alusi kuhusu hili amesema hivi: “Kwamba Amirul Mu’minin (A.S) alizaliwa ndani ya Kaaba ni jambo mashuhuri na linalojulikana duniani kote, na limetajwa katika vyanzo vya Kisunni na Kishia na kusisitizwa. Hali na miujiza ya mtu yeyote haijawa maarufu midomoni mwa watu wote kama yake, kiasi kwamba ulimi unashindwa kueleza sifa zake. Yeye ambaye ni Imamu na kiongozi wa Maimamu wote, anastahili kuwa kibla cha waumini wote. Ametakaswa na yule Mola ambaye ni Mwamuzi wa waamuzi wote, na ameweka kila jambo katika mahali pake sahihi.”[14]
- Ibn Fattal katika “Raudatul Wa’izin”, Al-Allamah Al-Hilli katika “Kashful Yaqin” na “Kashful Haqq” na Abu Muhammad Hassan Al-Dailami pia kutoka “Bisharatul Mustafa” katika “Al-Irshad” wote kwa pamoja wamepokea tukio hili.[15]
- Muhammad Salih Al-Tirmidhi, katika kitabu chake “Al-Manaqib Al-Murtadhawiyyah” ameleta muhtasari wake.[16]
- Sheikh Al-Saduq (aliekufa mwaka 381 Hijiria) amelitaja tukio hili katika “Al-Amali”, “Ilalush Shara’i'” na “Ma’anul Akhbar” kwa mabadiliko kidogo.[17]
- Al-Allamah Al-Amini naye katika kitabu chake chenye thamani kubwa “Al-Ghadir” ameleta vyanzo na maoni ya Kisunni na Kishia kuhusu kuzaliwa kwa Amirul Mu’minin (A.S) ndani ya Kaaba. Pia ametaja majina ya washairi walioashiria tukio hili katika mashairi yao.
- Baadhi ya vyanzo vya Kisunni vilivyotajwa viko hapa chini:
- 1- «Muruj Al-Dhahab 2», uk 2, kimetungwa na Abul Hassan Al-Mas’udi Al-Huzali.
- 2- «Al-Fusul Al-Muhimmah», uk 14, kimetungwa na Ibn Al-Sabbagh Al-Maliki.
- 3- «Al-Sirah Al-Nabawiyyah 1», uk 150, kimetungwa na Nuruddin Ali Al-Hanbali Al-Shafi’i.
- 4- «Sharh Al-Shifa Jz 1», uk 151, kimetungwa na Al-Sheikh Ali Al-Qari Al-Hanafi.
- 5- «Matunush Su’ul», uk 11, kimetungwa na Abi Salim Muhammad bin Talhah Al-Shafi’i.
- 6- «Muhadharatul Awa’il», uk 120, kimetungwa na Al-Sheikh Ala’uddin Al-Saktuwari.
- 7- «Miftahun Najah fi Manaqibi Ali Al-Aba», kimetungwa na Mirza Muhammad Al-Badakhshi.
- 8- «Al-Manaqib», kimetungwa na Al-Amir Muhammad Salih Al-Tirmidhi.
- 9- «Nuzhatul Majalis 2», uk 204, kimetungwa na Abdurrahman Al-Safawi Al-Shafi’i.
- 10- «Rawa’ihul Mustafa», uk 10, kimetungwa na Sadruffin Ahmad Al-Bardawani.
- 11- «Kitabul Hussein 1», uk 16, Al-Sayyid Ali Jalaluddin.
- 12- «Nurul Absar», uk 76, kimetungwa na Al-Sayyid Muhammad Mumin Al-Shablanji.
- 13- «Kifayatul Talib», uk 37, kimetungwa na Al-Sheikh Habibullah Al-Shanqiti.
Vyanzo
[1] AKHBARU MAKKAH 3, uk 226.
[2] AL-JALALI, WALIDUL KA’ABA, uk 186.
[3] AL-MUSTADRAK ALA AL-SAHIHAIN, Jz la Tatu, uk 550.
[4] AL-MARATIB, uk 60.
[5] AL-MANAQIB, uk 58.
[6] AL-NA’IMUL MUQIM, uk 129.
[7] TAZKIRATUL KHAWAS, uk 10.
[8] FARA’IDUS SIMTAIN, Jz la Pili, uk 425.
[9] TALKHISUL MUSTADRAK, Jz la Tatu, uk 550.
[10] TARIKHUL KHAMIS, Jz la Kwanza, uk 279.
[11] SHARH AL-SHIFA, Jz la Kwanza, uk 150.
[12] AL-SIRAH AL-HALABIYYAH, Jz la Kwanza, uk 154 na hapo hapo, Jz la Tatu, uk 405.
[13] IZALATUL KHAFA, Jz la Pili, uk 2512.
[14] Sharhul Kharidah fi Sharhil Qasidatil Ainiyyah, uk 15.
[15] Irshadul Qulub, uk 211.
[16] Manaqib Murtadhawi, chapa ya Bombay, uk 87.
[17] Al-Amali, Jz la Tisa, uk 114 na Ilalush Shara’i’, Jz la Kwanza, uk 3 na 135 na pia Ma’anul Akhbar, Jz la Goma, uk 62.