Yafuatayo hapa chini ni muhtasari wa wasifu na maisha ya Amirul Mu’minin (A.S).
“Kama moyo wako unamjua Mungu, tazama yote katika uso wa Ali; Nilimtambua Mungu kupitia Ali, naapa kwa Mungu.”
Jina: Ali bin Abi Talib (A.S)
Jina la Baba: Abu Talib, Abdu Manaf na Imran
Jina la Mama: Fatima bint Asad bin Hashim
Jina la Babu: Abdul Muttalib bin Hashim
Majina ya Kaka: Talib, Aqil, Ja’afar
Majina ya Dada: Ummu Hani, Jumana
Tarehe na Mahali pa Kuzaliwa: Amirul Mu’minin (A.S) alizaliwa siku ya Ijumaa, mnamo tarehe kumi na tatu ya mwezi wa Rajab ndani ya Kaaba Tukufu, miaka thelathini baada ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (S.A.W.W).
Kuingia Uislamu: Yeye ndiye mtu wa kwanza kusilimu.
Wake zake Maarufu: Fatima Al-Zahra (A.S), Umul Banin bint Hizam bin Khalid bin Darim Al-Kilabiyya, Layla bint Mas’ud Al-Darimiyya, Asma bint Umais Al-Khath’amiyya, Khawlah bint Ja’afar bin Qais Al-Khath’amiyya, Ummu Habib bint Rabi’ah, Ummu Sa’id bint Urwah bin Mas’ud Al-Thaqafi.
Watoto wa Kiume: Hassan (A.S), Hussein (A.S), Muhsin, Muhammad (mwenye lakabu ya Abu Qasim na anayejulikana kama Ibn Hanafiyya), Abbas (Abualfadhl), Amru, Ja’afar, Usman, Abdullah, Muhammad Al-Asghar (mwenye lakabu ya Abu Bakr), Ubaidullah, Auna na Yahya.
Watoto wa Kike: Zainab Al-Kubra (A.S), Zainab Al-Sughra (mwenye lakabu ya Ummu Kulthum), Ruqayya, Ummu Hassan, Ramlah, Nafisa, Ruqayya Al-Sughra, Ummu Hani, Ummu Kiram Jumana (mwenye lakabu ya Ummu Ja’afar), Umamah, Ummu Salama, Maimuna, Khadija na Fatima.
Lakabu za Kinasaba za Amirul Mu’minin (A.S): Abu Hassan, Abu Hussein, Abu Sabtain, Abu Raihanatain, Abu Turab; hii ni lakabu ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.W) alimpa Amirul Mu’minin (A.S).
Lakabu za Sifa za Amirul Mu’minin (A.S): Amirul Mu’minin, Murtadha, Wasiyyi, Haidar, Ya’asubul Muminina, Ya’asubuddin.
Sifa za Amirul Mu’minin (A.S)
1- Amirul Mu’minin (A.S) alizaliwa ndani ya Kaaba Tukufu, ambapo hakuna mtu yeyote aliyewahi kuzaliwa katika sehemu hiyo tukufu kabla yake.
2- Wakati ule ambapo Mtume (S.A.W.W) alipoanzisha udugu kati ya Waislamu, yeye mwenyewe aliweka agano la undugu na Amirul Mu’minin (A.S).
3- Yeye ndiye mshika bendera wa Mtume Mtukufu (S.A.W.W).
4- Mtume Mtukufu (S.A.W.W) alikuwa akimkabidhi Amirul Mu’minin (A.S) uongozi wa vita.
5- Amirul Mu’minin (A.S) alifikisha aya na maana za Surah Al-Tawbah kwa watu kwa niaba ya Mtume (S.A.W.W).
Bay’ah ya Amirul Mu’minin (A.S): Mnamo tarehe nane ya mwezi wa Dhul-Hijjah mwaka wa kumi Hijiria, huko Ghadir Khum kwa amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.W), watu walimpa baia Amirul Mu’minin (A.S) kwa ajili ya ukhalifa, lakini alifikia ukhalifa wa dhahiri mnamo Dhul-Hijjah mwaka wa 35 Hijiria.
Sehemu ya Ukhalifa wa Dhahiri: Kufa.
Washairi wa Amirul Mu’minin (A.S): Najashi, Al-A’awar Al-Shani.
Maandishi ya Kwenye Pete: Allahu Al-Malik wa Aliyyun Abduhu.
Vita: Jamal, Siffin, Nahrawan.
Bendera: Bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.W).
Athari: Nahjul Balagha.
Mwandishi: Abdullah bin Abi Rafi.
Shahada: Amirul Mu’minin (A.S) alianguka kitandani kufuatia pigo la “Abdurrahman bin Muljam Al-Muradi Al-Khariji” usiku wa kumi na tisa wa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka wa arobaini Hijiria, akiwa amesimama kuswali swala ya alfajiri katika msikiti wa Kufa, na alikufa shahidi usiku wa ishirini na mmoja wa mwezi huo huo.
Kaburi Takufu: Imamu Hassan (A.S) aliuzika mwili mtukufu wa Hazrat katika eneo la “Al-Ghari” au Najaf Al-Ashraf, na alilificha kaburi hilo kwa ajili ya taqiyyah kutokana na Makhariji na Muawiya, hadi leo hii ambapo kaburi takufu la Hazrat linashindana kwa utukufu na ukubwa na mbingu.