Sambamba na kumbukumbu ya shahada ya Imam Hassan al-Askari (amani iwe juu yake), Haram Tukufu ya Amirul Muuminiin (amani iwe juu yake) inawapokea wapenzi wenye nyoyo zilizojaa huzuni, waliokuja katika eneo hili tukufu kwa ajili ya kufanya maombolezi na kutoa rambirambi mbele ya Amirul Muuminiin (amani iwe juu yake), kiongozi wa wachamungu.








