Most searched:

Kuuawa kwa Bwana wa Mawasii katika Bwana wa Miezi

Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kila siku tunasikiliza kwa makini neno la thamani kutoka kwa Mkuu wa Ufasaha, Amirul Muuminina (a.s) kuhusiana na mwezi huu uliojaa baraka; ili nuru ya maneno yake matukufu iwe mwongozo kwetu katika kufaidika zaidi na baraka za mwezi huu wa utiifu kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa kuanza kwa mwezi wa mapenzi na ibada, mwezi mtukufu wa Ramadhani, hadithi kutoka kwa Amirul Muuminina Ali (a.s) kuhusiana na mwezi huu wa baraka zimekusanywa kwa ajili yenu, wasomaji waheshimiwa, na zitachapishwa kila siku chini ya anwani “Hadithi za Alawi” katika sehemu maalum ya Ramadhani Tukufu.

Hadithi ya siku ya ishirini na moja

Amirul Muuminina Ali (a.s) alisema:

«Nilimsikia mbora wa manabii, mitume na malaika waliokurubishwa akisema: “Hakika Bwana wa mawasii atauawa katika Bwana wa miezi. Nikauliza: ewe mtume wa mwenyezimungu ni upi bwana wa miezi na nani ndie bwana wa mawasii? Mtume akajibu: Ama Bwana wa miezi, ni mwezi wa Ramadhani, na ama Bwana wa mawasii, ni wewe, Ewe Ali!”»

سمعتُ أفضل الأنبياء و المرسلين و الملائكة المقربين يقول: إن سيد الوصيين يقتل في سيد الشهور، فقلتُ يا رسول الله و ما سيد الشهور و من سيد الوصيين؟ قال: أما سيد الشهور فشهر رمضان و أما سيد الوصيين فأنت يا علي!

Chanzo
Fada’il al-Ashhur al-Thalatha, Sheikh Saduq, uk. 108