Most searched:

Kutotumia Vibaya Madaraka na Wadhifa

Barua kwenda kwa Ash’ath bin Qais, gavana wa Azerbaijan, kimsingi inaashiria nukta hii kwamba vadhifa na madaraka katika serikali ya Kiislamu si njia ya kujipatia chakula na kipato kwa ajili ya mtu binafsi, bali ni amana za Mwenyezi Mungu ambazo ni lazima zilindwe kwa umakini mkubwa.

Matini ya barua hiyo ni kama ifuatavyo:

“Ugavana huu si njia ya kupata chakula na kipato kwako; bali ni amana shingoni mwako na (jua kwamba) unasimamiwa na aliye juu yako. Huna haki kabisa ya kufanya ukaidi na ukatili kwa raia, na huna haki ya kuingia katika mambo muhimu na hatari bila kuwa na uhakika. Mkononi mwako kuna sehemu ya mali ya Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka, na wewe ni mmoja wa watunza hazina Wake, ni lazima uilinde ili uifikishe mikononi mwangu, natumai sitakuwa kiongozi mbaya kwako, Wassalam.”

Chanzo

Barua ya tano kutoka Nahjul Balagha