Most searched:

Sherehe ya Maulidi ya Mtume Mtukufu wa Uislamu na Imam Swadiq (a.s.) katika Haram Tukufu ya Alawi

Watumishi wa Atabatul Alawiyya waliadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Hazrat Muhammad (swalla Allaahu alayhi wa aalihi) na Imam Swadiq (a.s.).

Watumishi wa Atabatul Alawiyya, sambamba na ziara ya asubuhi, waliandaa hafla kubwa katika Sahni ya Haram Tukufu ya Alawi kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Mtume wa Allah, Hazrat Muhammad (swalla Allaahu alayhi wa aalihi), na mjukuu wake mwenye heshima, Imam Ja’afar Swadiq (a.s.).

Hafla hiyo ilifanyika kwa usomaji wa kuvutia wa aya kutoka Qurani Tukufu, pamoja na nyimbo za kumsifu Mtume wa Allah (swalla Allaahu alayhi wa aalihi) na Ahlul Bayt wake watukufu (a.s.), katika hali iliyojaa utukufu wa kiroho na furaha.

Watumishi wa Haram ya Amirul Muuminiin (a.s.) pia walionyesha furaha yao kwa munasaba wa Maulidi haya yenye baraka kwa kugawa maua na peremende kwa mazuwaru katika Haram Tukufu ya Alawi.

Yaliyomo zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *